Na Abdullatif Yunus, Kasibante Fm.
Halmashauri  ya Wilaya Bukoba, Ipo katika Mkakati na Hatua za Awali  za kuyapeleka Makao Makuu ya Wilaya Bukoba, katika tarafa ya Rubale, Kata Rubale.
Hayo  yamebainika katika Mkutano wa Hadhala wa Wananchi pamoja na wadau wa Elimu, uliofanyika katika Kata ya Rubale Juni 3, 2017.
Akihutubia katika mkutano huo, Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukoba, Mh. Murshidi Hashim Ngeze amesema,  tayari  Halmashauri imekwishatuma timu ya Wataalamu kukagua maeneo wapi  panafaa kuwekwa Makao Makuu hayo ya Wilaya, Rubale ikiwa ni eneo mojawapo linalopewa kipaumbele, hivyo wananchi wawe tayari kuyapokea  maamuzi hayo pale yatakapopitishwa.
Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, Mwenyekiti Ngeze  amesema kuwa  tayari  mazungumzo ya awali yameanza kufanyika ikiwa ni pamoja na kuanza  mipango  ya kuanza kuifanya  Rubale kuwa Mji mdogo, huku akitoa Rai kwa Wananchi  kukubali usumbufu na uharibifu utakaojitokeza  kuhusiana na mali zao, kwani Maendeleo pia huambatana na hasara.
Awali mwenyekiti  Ngeze ambae pia ni Diwani wa Kata ya Rukoma, amewapongeza wananchi kwa kujitolea kuchangia vifaa vya ujenzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Rubale, na kuahidi kuendelea kutafuta wahisani mbalimbali ili kuchangia Ujenzi wa Shule hiyo, na kusisitiza kuwa Shule hiyo  ambayo inapendekezwa kuwa ya Wasichana  pekee ni lazima itajengwa Rubale.
Kwa upande wake Diwani wa viti maalumu Tarafa Rubale kupitia CCM,  Bi Asuma Kokugonza Bantanuka  amewaomba akina mama kujitokeza kwa wingi kuunga mkono Ujenzi huo, na kuwataka wnawake ikibidi kujitoa na kujitolea kufanikisha zoezi hilo, lengo likiwa ni kumsomesha mtoto wa kike kwa maendeleo ya Baadae.
Bi Asuma aliefuatana na Mwenyekiti Ngeze Katika ziara hiyo ameongeza kuwa, mwanamke ana nafasi na jukumu kubwa katika jamii hasa katika suala la maendeleo hivyo, hana budi kubaki nyuma ili kujikwamua kiuchumi.
 Diwani viti maalum Tarafa Ruabale - CCM Bi Asuma Kokugonza Bantanuka akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo..
 Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukoba, Mhe. Murshidi Hashim Ngeze akizungumza na hadhara iliyohudhuria mkutano wake eneo la Katani, Rubale.
Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakiendelea kufuatilia hotuba. 
Picha zote na Allawi Kaboyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...