Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siang'a (wa pili kulia) akiangalia sehemu ya kemikali bashirifu katika eneo la bandari kavu ya Ami Tabata jijini Dar es Salaam.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya imekamata kontena mbili zilizobeba kemikali bashirifu zilizokuwa tayari kwa kuingizwa nchini katika eneo la Bandari Kavu ya Ami Tabata Relini, Jijini Dar es salaam.


Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Kulevya , Rogers Siang’ a ameendesha operesheni  ya ukamataji wa Kemikali  bashirifu ambazo zilikuwa zikiingia nchini na kuanza kwa matumizi yake.



Akizungumza wakati wa  ukaguzi wa kemikali hizo, Kamishna Msaidizi wa Ukaguzi wa Kemikali Jinai ,  Bertha Mamuya, amesema  mzigo huo ni mwendelezo wa mzigo wa kampuni ya Tecno Scientific ambayo ilikuwa ikifanyia shughuli zake katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.

Amesema hapo awali waliweza kukamata lita 10,000  za Kemikali Bashirifu na katika Bandari ya Dar es Salaam zaidi ya  lita  6000 zimekamatwa zikitokea nchini Ufaransa.

Ametaja kuwa mamlaka inaendelea na uchunguzi wa kuzichunguza kemikali hizo hili kubaini kama zimefuata njia sahihi ya kuingia nchini na iwapo  itabainika kuwa Kemikali hizo zimeingia kinyume cha sheria wahusika watapelekwa mahakamani.
Baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), wakikagua kemikali ziliozopo ndani ya maboksi na kuchukua sampluli.
Mzigo wa kemikali bashirifu ukipakuliwa ndani ya kontena katika eneo la bandari kavu ya Ami tabata jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidzi wa ukaguzi kemikali jinai wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Bertha Mamuya
akiweka alama maboksi yaliyokutwa na kemikali bashirifu.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siang'a akiangalia mzigo wa kemikali bashirifu.
Mmiliki wa Kiwanda cha Tecno Scientific akiwa amekaa katika eneo la bandari kavu akiangalia mzigo wake unavyokaguliwa.
Wafanyakazi wa TRA na Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), wakikagua siri za kufungia kontena hili waweze kulifungua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...