Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MSTAHIKI  Meya wa Manispaa ya Ubongo, Boniface Jacob  amefanya kikao na wafanyabiashara wa Soko la Shekilango ili kuweka makubaliano ya maboresho ya soko hilo. 

Maboresho hayo ambayo yamelenga kuliweka soko la Shekilango na masoko mengine ya Manispaa ya Ubongo katika hadhi nzuri na kuongeza mapato kwa serikali.   

Akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo, Jacob amesema, maboresho ya soko hilo yametengewa Tsh milioni 50 ambazo ni mapato ya ndani ambayo  yaliyotokana na kodi zao. Amesema maboresho hayo yataanza baada ya siku 7, yatachukua siku 14 kukamilika na wafanyabiashara waliopisha marekebisho hayo kurudi sehemu zao za biashara.

Jacob amesema mara baada ya wafanyabiashara kurejea katika maeneo yao, makubaliano ya ushuru yatakuwa  baina ya Manispaa ya Ubungo na mfanyabiashara na siyo tena mfanyabiasha na mfanyabiashara.
"Nimekuja kuwasikiliza wafanyabiashara wote  sitaki kuwaletea njaa,nataka tuangalie hali ya sasa na mzunguko wa ela tangu 2000 na tukubaliane".

 Jacob amesema mara baada ya maboresho ya mabanda ya mbogamboga ambayo ushuru wake utapanda kidogo, awamu itayofuata itawagusa wapanga na wamiliki wa fremu 12 na vyoo ambao kwasasa wanalipa sh 200 kwa siku.

 Aidha Jacob aliwataka wamiliki wa fremu hizo kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa kufanya mazungumzo naye ili kupata makubaliano ya pamoja ya kisheria ili fremu hizo ziwe mali ya serikali na wao kulipia ushuru unaoendana na mahitaji ya sasa kiuchumi.
 Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Shekilango juu ya maboresho ya soko hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob akimununuza wafanyabiashara katika Soko la Shekilango alipotembelea soko hilo.
Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob akitembelea Soko la Shekilango  juu ya kulifanyia maboresho leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...