Taswira kabla ya kuanza kwa usafi wa fukwe ya Mbezi Beach ambapo ni fukwe inayotumiwa na wakazi wa Mbezi Beach na maeneo ya jirani , lakini kuna uchafu mwingi uliokusanyika pembeni hapo na kuleta kero kwa wakazi hao wanaotumia fukwe hii kwa mapumziko . 
Wadau na marafiki wa bahari wakiendelea kufanya usafi katika maeneo ya fukwe hii ya Mbezi Beach ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,Nipe Fagio na Marafiki wa Bahari na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita. 
Baadhi ya sindano zilizopatikana wakati wa usafi wa fukwe ya Mbezi Beach uliofanyika mapema mwishoni wa wiki iliyopita ,Sindano hizi ni hatari kwa watumiaji wa fukwe hasa kwa watoto wanaocheza bila kuwa na tahadhari. 
Taswira ya Fukwe ya Mbezi Beach wakati wa usafi ukiendelea .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...