MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya kutembelea maeneo ya katikati ya mji na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hasa wafanyabiashara ndogo ndogo.

Hatua hiyo ya Mavunde imetokana na Ofisi yake ya Mbunge kuweka utaratibu wa kuwasikiliza wananchi kero zao na matatizo yao kila Alhamis(kero za Ardhi) na Ijumaa(Mambo ya kijamii).

Hata hivyo kwa siku ya leo kutokana na mapumziko ya Sikukuu ya Eid El Fitr, Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ameamua kutembea maeneo mbalimbali ya mjini katikati na kusikiliza kero za wananchi.

Maeneo aliyotembelea ni pamoja na eneo la ‘One way’ ambalo kuna wafanyabiashara wengi wakubwa na wadogo na barabara ya sita ambako ni maarufu kwa maduka ya simu katika kata ya Madukani.

Akizungumza mara baada ya kuwatembelea wananchi hao, Mavunde ameahidi kuzipatia ufumbuzi baadhi ya kero zinazowasibu wafanyabiashara hao.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwasikiliza wafanyabiashara ndogo ndogo(machinga) katika eneo la ‘One way’.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyabiashara katika maduka ya simu barabara ya sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...