Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde amefungua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa kwa vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini.

Akizundua mpango huo katika karakana ya viatu na bidhaa za ngozi ya Taasisi ya Teknlojia ya Dar es salaam (DIT) tawi la  Mwanza, Mhe Mavunde, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana na pia kutumia bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo kwa ajili ya kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi nchini.

Amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya ujenzi wa viwanda kwa kuwajengea uwezo vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa katika kujiandaa na mfumo wa mapinduzi ya viwanda ambavyo vimeshaanza kujengwa nchini.
Aidha amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka kuwa kazi rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi, amewataka vijana kubadilisha mtazamo wa maaana ya Ajira kwa kutokukaa na kusubiri nafasi za ajira.Amesema mpango huu wa miaka mitano unalenga kuwafikia vijana zaidi ya milioni 4 nchini katika kuwajengea uwezo ambao utawafanya kujiajiri au kuajiriwa katika Tanzania ya viwanda.

 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akikagua ngozi zinazotumika kwenye mafunzo hayo katika Taasisi ya Teknlojia ya Dar es salaam (DIT) tawi la  Mwanza
 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akitembelea karakana ya Taasisi ya Teknlojia ya Dar es salaam (DIT) tawi la  Mwanza
 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akishuhudia sehemu ya vijana hao 1000 kutoka mikoa zaidi ya kumi wakijifunza namna ya kutengeneza viatu
Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde katika picha ya pamoja na vijana hao pamoja na wakufunzi wao. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...