Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amewaasa mawakili kutokuwa mawakala wa kupeleka rushwa mahakamani badala yake wawe mawakala wa kutenda haki na kufuata maadili ya sheria.

Aidha, amewaasa mawakili hao wasome zaidi sheria za nje ya Tanzania ili pindi wanapotayarisha mikataba iwe mizuri kwa kuwa mikataba mingi inayoingiwa haitegemei sheria ya hapa nchini pekee.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha mawakili 248 kutoka vyuo mbalimbali nchini, ambao wameingizwa katika orodha ya mawakili waliopo Tanzania.

Profesa Juma amesema Tanzania inaingia mikataba mingi ambayo haitegemei sheria zilizopo nchini, hivyo wanapaswa kusoma zaidi ili wanapoandaa mikataba hiyo iwe kwa maslahi ya taifa.Ameongeza kuwa, wananchi wengi wamekuwa wakitoa maoni yao kwamba kuna tatizo la rushwa mahakamani ambalo halipaswi kufumbiwa macho.

Amesema ni vema mawakili wakafuata sheria na kuwa na maadili ya kufanya kazi kwa weredi na na siyo kupeleka rushwa mahakamani.

Aidha amewaambia mawakili hao kuwa, karne ya hii ya sasa inawataka mawakili kutumia ujuzi wao wa sheria sio kutafsiri na kuelewa sheria za Tanzania pekee bali na za Kimataifa pamoja na kupambana na changamoto zinazoikabili nchi.

Profesa Juma amesema mapambano yao yanatakiwa kulenga kuondoa umasikini kwa kuwa wanasheria wa wanyonge na kuisaidia nchi kufikia malengo yanayotakiwa.

Pia amewaasa mawakili hao kuangalia gharama walizotumia wazazi wao hadi walipokubaliwa ili wawasaidie na kuisaidia serikali kutoka ilipo.

Hata hivyo, aliwatoa hofu mawakili hao kwamba Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), hakiwezi kufutwa kwa kuwa imependekezwa kuwepo kwa mabadiliko ya sheria ambayo hayalengi mtu wala taasisi binafsi bali inaangalia sheria kwa upana wake.

Alisema wanataka kuangalia mawakili wenye viwango, vyuo vinavyotoa sheria vinakidhi viwango hivyo hawapaswi kuwa na hofu.

"Tunatarajia vijana hawa wadogo walioapishwa leo wataweza kulitumikia taifa kwa zaidi ya miaka 30, katika umri wa kustaafu wa miaka hivyo tunategemea matokeo chanya kutoka kwao," ameeleza Kaimu Jaji.

Naye, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema mawakili hao ni wasaidizi wa mahakama katika kutenda haki na kwamba wanatakiwa kuielekeza jamii njia ya utawala wa sheria, haki za binadamu na demokrasia.

"Idadi ya mawakili Tanzania ni ya pili katika Afrika Mashariki ikiongozwa na Kenya na mwisho Uganda. Kuapishwa kwa mawakili hawa ni jambo jema ambalo Tanzania inajipanua katika utoaji wa huduma," alisema Lissu.

Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akifuatilia jambo wakati wa sherehe za 56 za kuwakubali na kuwasajiri, Mawakili wapya 248 mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya ndugu wa Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa kwa ndugu zao mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (wanne toka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji na Mawakili wapya mara baada ya kuwaapisha mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...