THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MBOGWE WAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI KWENYE GEREZA LA KANEGERE

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe wameadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti kwenye eneo la Gereza la Kanegere.
Akiongea baada ya kupanda miti Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji (W), Bi Furaha Chiwile amewataka wananchi  na watumishi  kwa ujumla kupanda miti kwa wingi na kuitunza na waepuke kukata miti ovyo  kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha mazingira na  vyanzo vya maji.

Jumla ya miti 200 ilipandwa lengo likiwa ni kupanda miche 2500 kwenye eneo hilo la magereza. Miche hiyo inayofadhiliwa na TASAF awamu ya tatu inapandwa kwenye Taasisi za serikali  wilayani  Mbogwe.

Wakati huo huo Afisa Mazingira wa Wilaya Charles  Karibu Tuyi alisema “ Kauli Mbiu ya Siku ya Mazingira    kitaifa ni Hifadhi Mazingira Mhimili kwa Tanzania ya Viwanda”. Amewashukuru watu wote waliojitokeza kupanda miti na amewaomba waonyeshe ushirikiano wa kuitunza  miti hiyo kwani itasaidia sana kutunza vyanzo vya maji.

Pamoja na  hayo ,Afisa  Mazingira (W)  alikabidhi jumla ya miche 920 kwa mwakilishi wa mkuu wa Gereza  Sgt. Kuyi  Kalulumila ambaye ameahidi kuitunza miche hiyo na amemshukuru Mkurugenzi kwa kulikumbuka gereza hilo kwani lina eneo kubwa na linauwezo wa kutunza miti hiyo.
 Afisa Mazingira (W) Charles Karibu Tuyi akipanda mti kwenye zoezi la upandaji miti ambalo kiwilaya lilifanyikia kwnye gereza la Kanegere wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 
 Afisa Mazingira(W) Charles Karibu Tuyi akimkabidhi Kaimu mkuu wa Gereza Kuyi Kalulumila miche ya miti inayotakiwa kupandwa kwenye Eneo la Gereza wakti wa Siku ya Mazingira Duniani.
Baadhi ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Wakiwa Wanapanda Miti na kuimwagilia.