Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini. 
MBUNGE wa Jimbo la Hai na Kionozi wa Kambi rasmi Bungeni Mhe Freeman Mbowe ametunukiwa cheti cha heshima na jamii ya Waislamu katika wilaya ya Hai kutokana na jitihada zake zisizo na ukomo katika kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali. 
“Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho. 
Mhe Mbowe alikabidhiwa cheti hicho na Mjumbe wa Baraza Kuu la Waisalmu (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa , katika msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge huyo kwa waumini wa misikiti minne tofauti ya Modio, Rundugai, Kibaoni na Lambo. 
Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Freeman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bi. Helga Mchomvu wakati wa Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti.
Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai Sheikh Omar Mohamoud akizungumza wakati wa hafla ya kupata Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Freeman Mbowe.

Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Freeman Mbowe akisalimiana na Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki Fahad Lema mara baada ya kuwasilisha ombi la kusaidiwa ujenzi wa vyumba vya madrasa ambapo Mh Mbowe alichangia kiasi cha shilingi milioni 2 kwa ajili ya kununua mbao za kuezekea Paa.  
Mbunge wa jimbo la Hai Mhe. Freeman Mbowe akisalimana na vijana waumini katika Msikiti wa Kibaoni uliopo Bomang'ombe wilayani Hai ,mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kupata futari iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Hai, Mhe Freeman Mbowe akipata Futari na waumini wengine katika Msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai baada ya kushiriki pia katika miskiti mingine mitatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...