Na Jumia Travel Tanzania
Siku ya Jumatatu ya Juni 5 itakuwa ni maadhimisho ya ‘Siku ya Mazingira Duniani’ ambayo huadhimishwa na mataifa tofauti duniani ikiwa imebeba kauli mbiu ya ‘Kuwaunganisha Watu na Mazingira Asilia.’ 

Mapema wiki hii Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba  alitoa taarifa kwa umma kuwa kwa hapa nchini maadhimisho ya siku hiyo kitaifa yatafanyika kijijini Butiama mkoani Mara, mahali alipozaliwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl. Julius Nyerere, ikiwa ni kuenzi jitihada zake za kulinda na kuhifadhi mazingira.

Katika kunogesha sherehe hizo Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa ofa kwa wananchi kutembelea hifadhi yoyote ya mbuga ya wanyama bila ya kiingilio chochote kwa siku tatu, kuanzia Ijumaa ya Juni 2 mpaka Jumapili ya Juni 4. Alisema kuwa lengo kubwa ni kuona uwepo wa wanyama na kujifunza kuwa mazingira yanahitaji kulindwa zaidi na zaidi.
Kauli hiyo ya Waziri imekuja siku chache baada ya kampuni inayojihusisha na masuala ya huduma za hoteli mtandaoni barani Afrika, Jumia Travel kuzindua kampeni ya ‘DemocratizeTravel’ inayolenga kuwakomboa waafrika na watanzania kiujumla katika kusafiri na kutalii vivutio mbalimbali nchini huku wao wakirahisisha huduma za malazi na hoteli.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...