MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku amewataka wananchi heri ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akiwataka kujiandaa na ujio wa fursa ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga kwa kuongeza uzalishaji. 

Alhaji Mussa aliyasea hayo wakati akizungumza na mtandano huu ambapo alisema mradi huo ni mkubwa ambao utahusisha watu wengi hivyo wananchi wanapaswa kujipanga ili kuweza kuendana na fursa hiyo muhimu kwa ajili ya kujiongezea kipato halisi.

Alisema lazima wakazi wa mkoa huo watambue kuwa wakati mradi huo ni mkubwa ambao unaweza kuchangia ukuaji wa kipato chao hivyo wajiandae kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo mama ntilie waweze kuendesha shughuli zao kisasa.

“Mkoa wa Tanga hasa kwenye Jimbo langu la Tanga mjini kutatekelezwa mradi mkubwa wa mradi wa boma la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hiyo wananchi wangu wajiandae kwa kuongeza uwajibika na uzalishaji ambao utakuwa na tija kwao “Alisema.

“Lakini pia niwaambie wenzetu madereva wa tax, mafundi wajiandae kikamilifu kuona namna ya kuboresha huduma zao kwani ujio wa mradi huo utalifanya Jiji la Tanga kuwa na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuweza kupata mafanikio “Alisema.

Aidha pia mbunge huyo aliwataka waumini ya dini ya kislaam kuendelea kutenda mema hata baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa ramadhani ikiwemo kuwajali wengine.

Mbunge huyo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wana sheherekea vema sikukuu ya Iddi Salama kwa kuwa makini hasa wakati watoto wao wanapokwenda kutembelea wawe na wasaidizi.


Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...