THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MBUNGE PANGANI AWATAKA WANANCHI KUWEKEZA KWENYE KILIMO ILI KUPATA MAFANIKIO

MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amewataka wananchi kuwekeza kwenye kilimo chenye tija kwa kuongeza uzalishaji ili waweze kupata mafanikio na kijikwamua kichumi. 

Aweso aliyasema hayo wakati akizungumza na Mtandao huu ambapo alisema wilaya ya Pangani imejaliwa kuwepo na ardhi yenye rutuba ambayo inaweza kustawisha mazao ya aina yoyote. Alisema kutoka na fursa hivyo wananchi wanapaswa kuitumia kama mtaji wa kuweza kulima kilimo chenye manufaa ambacho kinaweza kuwa mkombozi wao. 

Aidha pia alisema lazima wabadilike waona namna ya kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kwa kuongeza wigo mpana wa kujikita kwenye kilimo. 

“Mradi mkubwa wa bomba la mafuta hii ni fursa kubwa hivyo lazima wananchi wa Jimbo langu la Pangani waone ni vipi wanaweza kuitumia kwa kuongeza uzalishaji wenye tija na manufaa kwao “Alisema. 

Hata hivyo aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kushikamana kwa pamoja ili kuweza kupata maendeleo ikiwemo kuongeza bidii katika kuzalisha mazao mbalimbali yanayolimwa na kustawi vizuri. 

Hata hivyo aliwataka kulinda maeneo yao na kuacha kuyauza jambo ambalo linaweza kuwarudisha nyuma kimaendeleo na kujikita wakishindwa kuendana na ujio wa fursa mbalimbali ikiwemo mradi wa bomba la mafuta. 

“Ndugu zangu wananchi wanaweza kutokea watu wakawarubuni muwauzie maeneo yenu niwaambie tu achane kuuza maeneo yenu ovyo kutokana na ujio wa fursa hiyo muhimu “Alisema.
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza na Wananchi.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.