Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Koka, alisema kuwa alifanikiwa kupata msaada wa vifaa hivyo kutoka kwa rafiki zake waishio nchini Marekani, wakati alipokwenda katika shughuli zake za kibiashara, ambapo walimhakikishia kupata vifaa hivyo kwa kuchangia gharama za usafirishaji hadi kuingia nchini.

Baada ya uhakika huo Koke alitumia gharama zake kuwasafirisha baadhi ya wataalamu (Wazungu) kutoka nchini Marekani na kuja nchini hadi Mji wa Kibaha kwa lengo la kukagua na kujiridhisha juu ya uhitaji wa vifaa hivyo vya kutolea huduma za afya, ambapo alitumia jumla ya Sh. milioni 12.

Aidha alisema kuwa vifaa hivyo vilichelewa kutokana na uhitaji kutoka mataifa mengine yaliyokuwa yakipata matatizo na magonjwa ya mlipuko, na hivyo kampuni hiyo ya Project Cure, kulazimika kughairisha kusafirisha kuja nchini na kutoa kipaumbele kwa mataifa hayo yaliyokuwa yakipata matatizo kwanza.

Mbali na Mbunge kuchangia kiasi cha Sh. milioni 12, pia Halmashauri ya Mji wa Kibaha pia ilichangia kiasi cha Sh milioni 32, zilizosaidia kusafirisha vifaa hivyo kutoka nchini Marekani hadi kuwasili nchini. Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa hii leo vina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 400.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa tano kushoto) akipokea karatasi yenye orodha ya Vifaa vya kutolea huduma za Afya kutoka kwa Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kushoto kwake) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 400 iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya Mkoani, mjini Kibaha, leo mchana. Kulia kwa Waziri ni MKuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akikagua sehemu ya vifaa hivyo wakati akikabidhiwa na Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kulia kwake).
Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya kutolea huduma za Afya, iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mjini, Asumta Mshama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...