Mbunge wa Mufindi mjini Mhe. Cosato Chumi akikabidhi ambulance kwa ajili ya kituo cha Afya cha Ihongole .
 Mbunge wa Mufindi mjini Mhe. Cosato Chumi akikabidhi vitanda kwa wanafunzi  wa shule ya Sekondari ya Isalavanu wilayani Mufindi mkoa wa mkoani Iringa
 Hii ndio hali ilivyokuwa kwa Wanafunzi  wa shule ya Sekondari ya Isalavanu wilayani Mufindi mkoa wa mkoani Iringa ambao walikuwa wanalala kwa kutandika magodoro sakafuni. Zishukuriwe jitihada za Mbunge wa Mufindi mjini Mhe. Cosato Chumi ambaye kwa kushirikiana na  wadau wake wa maendeleo amekabidhi vitanda 35 aina ya double decker kuondoa adha hiyo. Aidha Mbunge Cosato Chumi pia amekabidhi ambulance kwa ajili ya kituo cha Afya cha Ihongole, na kusema "Asante sana Mhe Ummy Mwalimu na Uongozi mzima wa Wizara ya Afya wana-Mafinga tunasema asante sana".
 Wanafunzi  wa shule ya Sekondari ya Isalavanu wilayani Mufindi mkoa wa mkoani Iringa wakimshangilia Mbunge wa Mufindi mjini Mhe. Cosato Chumi wakati anashusha vitanda vyao
Vitanda 35 aina ya double decker vikiwa vimewasilishwa shuleni hapo na Mbunge wa Mufindi mjini Mhe. Cosato Chumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...