Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MFANYABIASHARA wa Kariakoo, Casto  Ngogo (35) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na nguo za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) za milioni 50.

Ngogo ambaye ni Mkazi wa Tabata Segerea amefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa na kusomewa mashitaka yake na Inspekta msaidizi wa polisi Hamisi Saidi.

Imedaiwa kuwa, Juni 15, mwaka huu maeneo ya bandari kavu ya Galco iliyopo Chang'ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Ngogo alikutwa na suruali 5,000 za JWTZ kwenye kontena namba PCIU 82851 (5) zenye thamani ya Sh milioni 59 mali ya serikali bila kuwa na kibali.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana  baada ya kutimiza masharti ya dhamama.

Akisoma masharti hayo ya dhamana, Hakimu Nongwa amemtaka mshitakiwa  kuwasilisha fedha taslimu  milioni 30 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo pamoja na wadhamini wawili watakaosaini ahadi ya milioni 10 kila mmoja.

Kesi imeahirishwa hadi Julai 17 mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi bado haujakamilika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...