Wakazi wa mwanza wameaswa kuendelea na utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara pamoja na kujiunga katika vikundi mbalimbali vinavyohusiana na michezo  kwa manufaa ya afya zao. Wito huo umetolewa na Afisa utawala wa wilaya ya Ilemela Mr. Saidi Kitinga katika uzinduzi wa  kikundi cha EFM jogging Mwanza, uliofanyika siku ya Jumamosi tarehe 10/06/2017 katika kiwanja cha Furahisha.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na vikundi mbalimbali vya mbio za mwendo pole (Jogging) za mkoa huo pamoja na maafisa kutoka katika ngazi ya wilaya na mkoa.
Efm redio kupitia kikundi chake cha Jogging inatarajia kuhamasisha jamii umuhimu wa mazoezi katika kila mkoa ambao redio itafika, na kuhakikisha jamii inanufaika kupitia mazoezi.
 Wakaazi wa mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Kikundi cha Efm katika mbio za mwendo pole
 Wakaazi wa mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Kikundi cha Efm katika mbio za mwendo pole
 Mazoezi ya viungo katika uwanja wa Furahisha – Mwanza
Kulia ni Meneja Mkuu wa Efm redio Dennis Busulwa pamoja na Maulid Kitenge Mtangazaji wa Efm redio kipindi cha michezo
Meneja Mkuu Efm redio Dennis Busulwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...