THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Mkulima wa Handeni Tanga ajinyakulia Sh Milioni 20 za Biko


MAMBO yamezidi kunoga katika bahati nasibu ya ‘SMS’ ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, baada ya mkulima kutoka wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis, kuibuka kidedea kwa kuzoa Jumla ya Sh Milioni 20 kutoka kwenye bahati nasibu hiyo inayozidi kushika kasi nchini Tanzania, ikiwa ni droo yake ya 15 tangu kuanzishwa kwake.

Bahati nasibu hiyo imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba bahati nasibu yao imezidi kupanua mbawa zake kwa kutua wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa mshindi wao Yahaya ambaye ana umri wa miaka 50 anayejishughulisha na kilimo.

Alisema ni faraja yao kuona mchezo wao umekuwa ukitoa washindi katika sehemu mbalimbali za Tanzania, akiamini kuwa ni mwendelezo wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaibuka na mamilioni ya Biko.

“Tunafarijika sana kuona mkulima wa Handeni Tanga naye ameibuka na mamilionin ya Biko, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kumpatia utajiri mkubwa kwa kuzitumia fedha hizi kwa umakini katika shughuli zake za ukulima, ukizingatia kuwa amepatikana kwa kucheza Biko ambao ni mchezo rahisi kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku kiasi cha kucheza kikianzia Sh 1000 na kuendelea.


Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania, Humud Abdulhussein kushoto, akiagana na Balozi wa Biko, Kajala Masanja mara baada ya kumaliza kuchezesha droo ya 15 leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkulima wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis aliibuka kidedea kwa kuzoa jumla ya Sh Milioni 20.

Balozi wa Biko Kajala Masanja akichezesha droo ya 15 ya Bahati Nasibu ya Biko ambayo donge nono la Sh Milioni 20 liliangukia kwa mkulima wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis baada ya kuchezeshwa droo hiyo jana, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA