Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 13, 2016 amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba Jijini Dar es salaam kujionea hali ya Miundombinu ikiwemo majengo ya shule na ufanisi wa utoaji elimu katika Shule hiyo.


Mara baada ya kuzuru katika Shule hiyo Mkurugenzi Kayombo amebaini kuwapo na ubovu wa madarasa hivyo kuamua kujenga madarasa mengine mapya matano kwa ajili ya wanafunzi kujisomea kwa uhuru na amani shuleni hapo.



Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba vitano vya madarasa utaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.



MD Kayombo alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa madarasa hayo yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia amesema ujenzi wa madarasa hayo utakuwa wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya ubora wa majengo ya serikali.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza jambo mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (kushoto) na Afisa Uchumi Mkuu Ndg Yamo Wambura wakikagua majengo ya shule ya msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba wakati wa ziara ya kikazi
Madarasa manne yaliyoamuliwa kuvunjwa na kujengwa upya madarasa mengine matano katika Shule ya Msingi Hondogo Jijini Dar es salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...