RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekutana na Brigedia Jenerali
Fadhil Omar Nondo aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha baada
ya kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Brigedi
ya Nyuki Zanzibar.
Dk. Shein alitumia fursa
hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
ambaye pia, ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kwa kumteua Brigedia
Jenerali Fadhil Omar Nondo kushika wadhifa na kumpongeza Brigedia huyo huku
akimuhakikishi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wake itampa
mashirikiano makubwa kama ilivyofanya kwa viongozi waliokuwepo kabla yake.
Nae, Brigedia Jenerali Nondo
alimuahidi Dk. Shein kuwa ataendeleza uhusiano na ushirikiano mwema ulipo kati
ya Majeshi ya Ulinzi Tanznia pamoja na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huku akisifu mashirikiano mazuri anayoyapata
kutoka kwa viongozi wa Serikali na viongozi wa vikosi vya ulinzi vya SMZ na
kuahidi kutoa ushirikiano kwao pamoja na kwa wananchi wote wa Zanzibar.
Brigedia Jenerali Fadhil
Omar Nondo anashika nafasi ya Marehemu Bregedia Jenerali
Cyril Ivor Mhaiki, aliyekuwa Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar, ambaye
alifariki dunia tarehe 13, Disemba mwaka 2016 huko katika Hospitali ya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania, Lugalo jijini Dar-es-Salaam na kuzikwa Mkoani kwao Ruvuma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo baada ya mazungumzo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar
(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...