Na Jumbe Ismailly, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk.Rehema Nchimbi ameahidi kuvifuta vyama vya msingi vya wakulima wa zao la Tumbaku pamoja na Bodi ya Tumbaku ya Mkoa wa tumbaku Manyoni endapo wakulima wa zao hilo watakosa soka la kuuzia tumbaku yao waliyolima kwa mwaka 2016/2017.

Akifungua soko la zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa 2016/2017 uliofanyika katika Chama cha Ushirika cha Msingi Isingiwe LTD Mitundu,Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kwamba endapo wananchi hao watabaki na zao la tumbaku ndani ya nyumba zao,mwenyekiti wa Bodi ya tumbaku ndiyo itakuwa mwisho wa kuitumikia nafasi hiyo.

“Wananchi hawa wakibaki na tumbaku ndani nasema kabisa Bodi ya tumbaku hapa Mwenyekiti ujue kabisa uenyekiti wako haupo,ndiyo, kabisa kwa hiyo hii risala mliyonisomea hii tena mngesema afadhali tusingesoma na kuongeza….. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi (mwenye kufunga kitambaa kichwani) akipokea taarifa ya uteuzi wa madaraja ya tumbaku kutoka kwa mteuzi wa zao hilo,Bwana Charles Kizighaaliyevaa sare ya bluu).

Wanabaki na tumbaku hawa wananchi bila kupata soko vyama vya msingi hamna kazi,hamna kazii,lakini najua Mrajisi msaidizi ambaye ndiyo mlinzi na mlezi wa vyama hivi utahakikisha unasimama kwamba vyama hivi vikae vizuri na viendeleze heshima yake”alisisitiza.

Hata hivyo Dk.Nchimbi aliwataka watendaji,hususani maafisa ugani katika Halmashauri ya Itigi kujenga utamaduni wa kuishi na wakulima wa zao la tumbaku badala ya kuwatembelea pale tu wanapohitaji michango ya shughuli mbali mbali za mandeleo.
Marobota ya tumbaku yakiwa kwenye ghala la kuhifadhia tumbaku kabla ya kufanyiwa uteuzi wa madaraja na mteuzi wa zao hilo kutoka katika Bodi ya Tumbaku.

Katika risala ya wakulima wa zao la tumbaku wa vyama vitano iliyosomwa kwenye sherehe na Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika cha Isingiwe,Daud Ngayaula imevitaja vyama vitano vilivyolima zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa 2016/2017 kuwa ni pamoja na IsingiweAmcos,Manyanya Amcos,Idodoma Amcos,Mtakuja Amcos na Umoja Amcos.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Isingiwe Amcos alibainisha kwamba vyama hivyo vinatarajia kuzalisha kilogramu 295,000 ambazo iwapo zitanunuliwa zote kwa wastani wa bei ya kitaifa ya dola mbili za kimarekani kwa kilo,vyama hivyo vitapata dola 590,000 za zenye thamani ya shilingi 1,298,000,000/= za kitanzania.
baadhi ya wakulima wa zao la tumbaku kutoka katika vyama vitano vinavyolima tumbaku katika kata ya Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

Hata hivyo Ngayaula hakusita kuzitaja baadhi ya changamoto zinazovikabili vyama hivyo kuwa ni kupewa uzalishaji mdogo wa Makampuni na kujitoa kwa Kampuni ya AOTTL kutonunua zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa 2017/2018.

Naye Mteuzi wa zao hilo kutoka Bodi ya tumbaku,Charles Kizigha alisema katika siku ya kwanza ya ufunguzi huo wa soko tumbaku iliyonunuliwa ina thamani ya dola za kimarekani 575.786 sawa na shilingi za kitanzania milioni 1,281,085.13 kwa bei ya shilingi 2,225. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...