THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke kufanya oparesheni maalum kwa wadaiwa sugu

Kufuatia wafanyabishara kutokulipa kodi kwa wakati na wengine kuwa wadaiwa sugu na kupelekea baadhi ya halmashauri kukwama katika kuendeleza miradi ya maendeleo na kujitegemea hatimaye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kufanya oparesheni maalum kwa wadaiwa sugu.

Akizungumza mapema leo DC Lyaniva ameeleza kuwa zoezi hilo litalenga kukusanya kodi kwa wale wadaiwa sugu ambao wamekuwa wakidaiwa na Halmashauri hiyo kwa muda mrefu.

DC Lyaniva ametaja idadi ya wadaiwa sugu kuwa ni 142 ambapo wadaiwa wa leseni za biashara wakiongoza kwa idadi kubwa ya wadaiwa 69, ushuru wa huduma 52 na wadaiwa sugu kwa upande wa masoko wakiwa ni 21.

Jambo ambalo limepelekea halimashauri hiyo ya wilaya ya Temeke kutofikia malengo ya makusanyo ya kodi ya shilingi bilioni 29 ambapo wamefanikiwa kukusanya bilioni 23 pekee huku zaidi ya bilioni 6 zikibakia kwa wadaiwa sugu.

DC Lyaniva amesisitiza kuwa kwa wasiolipa kabla ya tarehe mosi ya mwezi Julai mwaka huu watachukuliwa hatua kali za kisheria, hivyo ni vyema wakatimiza wajibu huo haraka iwezekanavyo na kufafanua kuwa kwa umuhimu wa jambo hilo ofisi zitakuwa wazi mpaka siku ya jumapili.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva.