THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MSIUZE hOVYO CHAKULA KABLA YA KUWA NA AKIBA YA KUTOSHA- RC TABORA

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Wakazi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuweka akiba ya chakula cha kutosha ili kuepuka njaa inayoweza kuwakabili kutokana na mavuno ya msimu huu kutokuwa mazingira kufuatia mvua kuchelewa kuanza na kuwahi kukatika.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa kilele cha maadhimisho siku ya mazingira duniani ambapo kimkoa yalifanyika katika Manispaa ya Tabora.

Alisema mvua za msimu huu zilikuwa kidogo na hivyo mavuno ya mazao kama vile mahindi , mpunga na maharagwe ni hayaridhishi hivyo ni vema wananchi wakahakikisha wanatenga chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi yao kabla ya kuanza kuuza.

Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mikoa mbalimbali wamekuwa wakipita katika maeneo mbalimbali ya vijiji na kuwarubuni wakulima wawauzie mahindi yao nao bila kuchukua tahadhari wanafanya wamekuwa wakiuza bila kuweka akiba ya kutosha jambo ambao sio jema.

Aliongeza kuwa watu aina hiyo ambao wanakimbilia kuuza mahindi yao bila kuweka aakiba ya kutosha kwa ajili ya familia zao ndio wamekuwa wakimbilia kwa viongozi wa Serikali wanaishiwa chakula.

Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa ameamua kuwatahadharisha mapema ili kila mkazi wa Tabora akatumia fursa hii ya upatikanaji wa vyakula vya kutosha katika masoko kuweka akiba kwa ajili ya familia zao badala ya kukaa ili kugonja msaada na wakati mwingine kulaumu Serikali bila sababu za msingi.