Muft Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amewataka watanzania na waislamu kwa ujumla kupendeza kwa kuvaa mavazi yanayotengenezwa na kampuni ya mzawa Mussa Bakari ya 'Islamic Fashion Tanzania'. 

Kiongozi huyo waislamu nchini ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam Jumapili wakati akizindua kampuni hiyo ya mavazi ya kiislamu na kueleza kuwa kwa mujibu wa maandiko ya dini hiyo, wameamrishwa kupendeza kwani Mungu ni mzuri na na hupenda vitu vizuri. 
Mufti alifafanua kuwa uislamu huambatana na usafi na usafi huo unaanzia kwenye mavazi, hivyo ni vyema waislamu wakaitumia fursa hiyo kwa kununua mavazi kutoka kwenye kampuni hiyo ya mzawa. 
Pia ameishauri kampuni hiyo kujitangaza zaidi kwani hitaji wa vazi hilo ni mkubwa nchi nzima na sio tu kwa mkoa wa Dar es Salaam, na akawaomba watume muwakilishi kwenye sherehe za Eid El Fitr zinazotaraji kufanyika Mkoani Kilimanjaro kitaifa, ili wakazitangaze bidhaa zao na huko. 
"Ni vyema pia waislamu wakaambizana habari njema za ujio wa Islamic Fashion Tanzania ili wengi waweze kunufaika kwa kupendeza na mavazi yao" alisema Mufti Mkuu. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Islamic Fashion Tanzania Mussa Bakari ameeleza kuwa kampuni hiyo imeanza tangu mwaka 2014 ambapo walikuwa wanategemea mavazi hayo kutoka nchi za nje, kutokana na kwa jitihada walizofanya \ sasa wameweza kutengeneza mavazi yao ambapo nusu ya uzalishaji inafanyika Dubai na kumalizikia Tanzania.
Mkurugenzi Mussa Bakari ameongeza kuwa changamoto ya Watanzania kukosa kanzu zenye ubora kwa muda mrefu ndiyo zimewapelekea wao kuanzisha Islamic Fashion Tanzania, ili kuwarahisishia watanzania waliokuwa wanasafiri kwenda nje ya nchi wapate kanzu zenye ubora. Hivyo amewaomba watanzania kumuunga mkono ili aweze kupiga hatua zaidi za kuwahudumia watanzania.
 Muft Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir (kulia) akizungumza jijiini Dar es Salaamn wakati uzindui wa mavazi yanayotengenezwa na kampuni ya mzawa Mussa Bakari ya 'Islamic Fashion Tanzania.  
 Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Islamic Fashion Tanzania Bw. Mussa Bakari akiwaomba watanzania kumuunga mkono ili aweze kupiga hatua katika uzindui huo.
 Muft Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir (kulia) akizindua mavazi yanayotengenezwa na kampuni ya mzawa Mussa Bakari ya 'slamic Fashion Tanzania  kwa kushirikiana Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Sheikh Alhad Mussa Salim (katikati) na  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo  Bw. Mussa Bakari.
 Sehemu ya viongozi  na  wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
 Sehemu ya viongozi na wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.Picha na Emmanuel Maasaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...