Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubery Ali amesema kwamba mwenye mamlaka ya kutangaza mwezi ni ya Mufti Mkuu baada ya kushauriana na Kamati ya Mwezi. Baada ya Mufti kujiridhisha ndipo Bakwata huutangazia Umma kuhusu kuandama kwa mwezi.  
Hivyo basi Mufti wa Tanzania amesema jana mjini Moshi kwamba leo Jumamosi Juni 24, 2017 kamati ya mwezi itaendelea kufuatilia kuandama kwa mwezi na ikiwa utaandama watautangazia umma kuwa Jumapili itakua Eid El Fitr na ikiwa hautoonekana basi itabidi kukamilisha siku 30 za mfungo wa Ramadhan na Eid kuswaliwa Jumatatu In Shaa Allah.

Mufti wa Tanzania,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali akiwa katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri (VIP) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo.
Mufti wa Tanzania ,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali akiwa na viongozi pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti wa Tanzania,Sheikh Aboubakary Zubery Ali.
Mufti wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ali akiwasili katika mmoja wa misikiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi. 
Mufti wa Tanzania,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali  akifungua kitambaa katika kuweka jiwe la Msingi kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jengo hilo litakalotumika kama Madrasa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...