Halila Tongolanga, mwanamuziki  mkongwe ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya  Muhimbili jijini Dar es salaam toka wiki iliyopita,  amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. 
Tongolanga (pichani alipotembelewa juzi na Katibu mtendaji wa BASATA Bw. Mungereza), aliyejipatia umaarufu kwa wimbo wa "Kila munu ave na kwavo" alikuwa amesafirishwa kutokea Ndanda kuja Muhimbili akihisiwa kuwa na matatizo ya figo. 
Jana Jumapili ililazimika kuanza kufanya jitihada za kupata daktari ambaye angemshughulikia kwa karibu zaidi, na daktari alipatikana ambaye aliahidi angeanza kufwatilia swala lake leo asubuhi lakini mapenzi ya Mungu yalikuwa tofauti. 
Juzi alinukuliwa akisema kuwa ana mengi ya kutaka kusema, lakini moja aliloweza kutamka ni kuwa yeye anajihisi ana kansa. alipoulizwa anajuaje hilo, kwa vile hajapimwa hakuwa na jibu
Wengi tutamkumbuka Tongolanga kwa wimbo wake wa Kimakonde aliouimba kwa mara ya kwanza akiwa na Les Mwenge 'Kila Munu Ave Na Kwavo", na baadaye akafanya remix na Makondeko band.
Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa leo saa tano kuelekea kwao Newala kwa mazishi. Habari zaidi zitawafikia kupia hapa
Mungu amlaze Pema peponi Halila Tongolanga 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...