Taarifa tulizopokea hivi punde zinaeleza kwamba mmoja wa wanamuziki nguli nchini, Shaaban Dede, amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa msemaji wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), Dede amelazwa wodi ya Mwaisela Namba 5 kitanda namba moj, ambapo wadau wa muziki wameombwa kwenda kumjulia hali huku wakimuombea apate nafuu haraka. Taarifa hiyo haikumesema Dede anasumbuliwa na matatizo gani.

Shaaban Dede ni mwanamuziki mkongwe ambaye anajulikana kwa sauti yake tamu pamoja na tungo zilizosheheni kila aina ya ladha.

Kwa ufupi Dede alizaliwa Mkoa wa Kagera mwaka 1954 ambako alianza kupenda muzikiakiwa bado mdogo kabisa na bendi yake ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa ni ya TANU ambayo makazi yake yalikuwa Biharamulo, mjini Bukoba.
“Mwaka 1974 alijiunga na Bendi ya Polisi na mwaka 1975 akajiunga na Tabora Jazz ambako alikaa kidogo kabla ya kuhamia 1976 nilihamia Dodoma Internationl Band mwaka 1976  ambako alidumu kwa miaka mitatu.
Mnamo mwaka 1979 alijiunga na bendi ya Msondo wakati huo ikijulikana kama JUWATA JAZZ  ambako alidumu  mpaka mwaka 1982 alipoahamia Mlimani Park Orchestra wana SIKINDE ambako alikaa kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Bendi ya Bima a.k.a BIMA LEE. Mnamo  mwaka 1987 Deded alirudi tena Msondo ambako alikaa  kidogo na baadaye akahamia tena Sikinde. Hata hivyo mwaka 20111 akarejea tena Msondo ambako yuko hadi hii leo.
Globu ya Jamii inamtakia apate nafuu haraka gwiji wa muziki Shaaban Dede. Tutaendelea kuwaletea taarifa za maendeleo yake kila zitapopatikana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...