Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco Bitaho (54) amepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma tatu zikiwemo za kuishi na kufanya kazi nchini bila kibali.

Mshtakiwa Bitaho amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Akisoma hati ya mashtaka leo, wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji, Novatus Mlay amesema, Mei 19, mwaka huu huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji Bitaho akiwa raia wa Burundi alikutwa nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi nchini.
 
Aidha imedaiwa kuwa, siku na mahali hapo Mshtakiwa Bitaho alikutwa akifanya kazi kama mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.
 
Katika shtaka la tatu Mlay amedai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo wilaya ya Ilala, mshtakiwa akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba pasi ya kusafiria namba CT (5)(Ai).
 
Wakili Mlay aliongeza kuwa, kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Bitaho kupata pasi ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.
Hata hivyo mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
 
Mahakama imeamuru mshtakiwa Bitaho kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini dhamana ya milioni 20,na Kesi hiyo itatajwa tena Juni 21.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...