THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MWENGE WA UHURU WAACHA HAMASA KITUO CHA WATU WALIOATHIRIKA NA DAWA ZA KULEVYA SOBER HOUSE

Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru , Amour Hamad Amour amewaasa watendaji mbalimbali nchini kuwajali vijana kwa kuwapa fursa mbalimbali pale inapotokea.

Kiongozi huyo ameyasema leo wakati wa Mwenge wa Uhuru ulipopita katika mradi wa kituo cha watu walioathirika na Dawa za Kulevya Sober House Kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani,

Amesema kuwa vijana ndio wamekuwa waathirika wakubwa katika matumizi ya dawa za kulevya ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Nae Mkurugenzi Kituo hicho, Al –Karim Bhanji amesema vijana walioathirika na dawa za kulevya wanatakiwa kupewa upendo,kuwaacha kunaweza kukasababisha kurudi katika matumizi ya dawa za kulevya.

Bhanji amesema malengo ya kituo hicho ni kuwa na walimu ambao watakuwa wanawafundisha waathirika hao ili kurudi kuendesha biashara zao kutokana na elimu itakayotolewa na kituo hicho.

Amesema kuwa kutokana na kukua kwa sayansi na Teknolojia kituo kituo kitaanzisha darasa la kompyuta, ambapo waathirika watajifunza na wengine wanaweza kuwa na ujuzi tofauti.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga amesema kuwa Mwenge umetoa hamasa kubwa na kupelekea kufungua miradi mbalimbali ,ambapo Sober House ni mradi ambao umeokoa vijana wengi waliotumbukia kwenye matumizi ya dawa za Kulevya.
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru , Amour Hamad Amour (aliesimama) akizungumza na katika kituo cha Sober House wakati mwenge huo ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga (aliesimama) akizungumza wakati wa Mwenge wa Uhuru ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House , Al –Karim Bhanji (katikati)akizungumza jinsi wanavyoendesha kituo hicho wakati mwenge huo ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga
Mkurugenzi wa kituo hicho,Al –Karim Bhanji (katikati) akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru
Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd Amour akiwaaga viongozi na Watendaji wa Kituo hicho.
Mwenge wa Uhuru