THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson awajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpokea  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto  wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza jinsi wanavyotoa  huduma za matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimbembeleza mtoto Venance  Christopher (14) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kusubiri upasuaji wa  Moyo. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo   leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea jambo wakati akimjulia hali mtoto Rashid Kombo aliyelazwa katika  chumba cha uangalizi maalum (ICU) baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akifuatiwa na  Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto Dkt. Sulende Kubhoja. 
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto Godwin Sharau alipotembelea leo chumba cha upasuaji wa Moyo kilichopo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwetwe (JKCI). Picha na  Anna Nkinda wa JKCI.