Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Beki wa kati wa timu ya Nakuru All Stars James Sadicky Mukhwana amesema kuwa anaamini ipo siku atacheza katika mojawapo ya timu za ligi kuu nchini Tanzania.

Beki huyo mwenye mwili uliojazia n a urefu wa futi sita amesema kuwa anaitamani sana ligi ya Tanzania na kama ikitokea timu itakayomuhitaji yupo tayari kuitumikia ili mradi wakubaliane.

Mukhwana ambaye jana katika mchezo wa Nakuru All Stars dhidi ya Simba alionekana mwiba kwa safu ya ushambuliaji wa timu ya Simba na kuweza kuhakikisha hakuna mshambuliaji anayetikisa nyavu za timu yao.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26, amepitia katika timu mbalimbali za nchini ikiwemo kituo cha kukuzia vipaji cha Nakuru Youth Olympic mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 12 na baadae kupandishwa mpaka timu kubwa ya Nakuru All Stars na kuitumikia kwa miaka miwili.

Baada ya kuachana na Nakuru Mukhwana alijiunga na Complay Fc ya ligi daraja la kwanza mwaka 2013 na kuitumikia timu hiyo kwa mwaka mmoja na baadae kuhamia Osiria Fc mwaka 2014.

Mukhwana hakuweza kudumu sana katika timu ya Osiria na kujiunga na Bitiko United mwaka 2015 na kucheza kwa miezi sita na kuamua kwenda St joseph na kumalizia miezi sita iliyobaki ambapo zote zinashiriki ligi daraja la kwanza. Mwaka 2016, Mukhwana alijiunga na Nakumat na 2017 kuhamia Nakuru All stars ambapo anacheza mpaka sasa. 

Mukhwana amesema bado anaamini anauwezo wa kucheza mpira na anatamani sana kucheza ligi kuu ya Uingereza huku akisfia uwezo wa mchezaji raia wa Kenya Victor Wanyama anayekipiga katika timu ya Totenham, David Kalaba wa Zesco na mchezaji wa nje Thiago Silva. 

Nakuru wapo nchini kwa ajili ya michuano ya Sportpesa Super Cup inayoendelea ikizikutanisha timu nane ambapo kwa sasa umeingia katika hatua ya nusu fainali mechi zitakazopigwa kesho kati ya Yanga na AFC Leopard huku mchezo wa pili ukiwa kati ya Nakuru All Stars na Gor mahia.
Beki wa kati wa timu ya Nakuru All Stars James Sadicky Mukhwana akipambana na kiungo wa Simba Mohamed Ibrahim wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika michuano ya Sportpesa Super Cup.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...