MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu Mfanyabiashara Shabani Hussein (44) maarufu kama "Ndama mtoto ya Ng'ombe" kulipa faini ya milioni 200 au jela miaka mitano baada ya kukiri shtaka la sita la kutakatisha fedha ambazo ni dola za Marekani 540,000.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi, Mkuu wa mahakama hiyo Mhe. Victoria Nongwa.

Kabla ya hukumu hiyo kusomwa, upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Christopher Msigwa alimsomea maelezo ya awali (PH), Ndama dhidi ya shtaka lake hilo na kukiri.

Hatua hiyo ya Ndama kusomewa hukumu katika shtaka moja tu la utakatishaji wa fedha kati ya matano yanayomkabili limekuja baada ya wiki iliyopita kuomba kukumbushiwa mashtaka yake na kukiri shtaka hilo la utakatishaji wa fedha.
Akisoma hukumu hiyo, hakimu Nongwa amesema mahakama imezingatia hoja za upande wa mashtaka na ule wa utetezi ambapo upande wa mashtaka uliiomba mahakama kwa mujibu wa sheria ya kutakatisha fedha kifungu cha 13 (a)cha Sheria ya kuzuia utakatishaji fedha, kumpa adhabu kali mshitakiwa kwa kuwa makosa hayo yanalenga kudidimiza uchumi wa nchi.

Amesema, mshitakiwa anastahili faini kwa kuwa ameipunguzia garama mahakama kuhusu shughuli za uendeshaji wa kesi hiyo ikiwemo gharama za kuleta mashahidi katika shtaka hilo.
Ameongeza kuwa, Sheria hiyo ipo kwa ajili ya kuonesha kuwa makosa kama hayo hayatakiwi kumnufaisha mkosaji, hivyo atatakiwa kulipa faini ya milioni 200 na asipolipa ataandikiwa hati ya kifungo cha miaka mitano jela.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...