Jeshi  la Magereza jana Jumapili limemkamata kijana mmoja aitwaye Ramadhani Nombo akiwa na simu tano alizozificha kwenye mapande ya nyama aliyokuwa amepelekea ndugu yake/zake  mahabusu katika gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za jeshi hilo, hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.

“Kutokana na umakini wa askari wetu,  mara tu alipofika Keko na kuomba kuwaona ndugu zake walio mahabusu na kuwapa chakula walibaini kwamba ndani yake kuna simu” imesema taarifa hiyo. Haikutajwa nyama na hizo simu alikuwa anapalekewa  mahabusu gani hapo gerezani.

Taarifa zinasema kimsingi kijana huyo amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria ya Magereza sura ya 56 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 ambayo inakataza mtu yeyote kuingiza magerezani kitu chochote kisichoruhusiwa.
Kifungu hicho kinatamka bayana kwamba endapo ikithibitika mtu yeyote amekamatwa na kuingiza kitu chochote ambacho hakiruhusiwi kuingizwa gerezani, atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita (6) gerezani au faini au vyote kwa pamoja.

 Mtuhumiwa Ramadhani Nombo akiwa amebeba mapande ya nyama ambayo yanatuhumiwa kuwa na simu tano ndani yake 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...