Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Baada ya kuachiwa huru juzi na kukamatwa tena, leo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Bitaho (54) amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 13.9 au kifungo jela miaka mitano baada ya kusomewa upya mashtaka na kukiri.

Bitaho amefikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi na kusomewa mashitaka nane likiwemo la kufanya kazi nchini bila kibali na kutoa taarifa za uongo.

Bitaho ambaye ni Raia wa Burundi, alifutiwa mashtaka yake, na baadae kukamatwa,  amesomewa hukumu hiyo,  na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Akisoma hukumu hiyo Nongwa amesema kuwa mahakama imesikiliza maombi ya pande zote mbili na kwamba katika kosa la kwanza hadi la saba mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh laki tano au kifungo jela kuanzia miaka miwili hadi mitatu na kwamba kosa la nane mshitakiwa atatakiwa kulipa  faini ya Sh milioni 10 au kifungo jela miaka mitano.
Amesema, kwa taratibu zilizopo, baada ya mshitakiwa kukutwa na hatia anatakiwa kupelekwa Uhamiaji na kurudishwa nchini kwao ili aombe uraia wa Tanzania upya.
Kabla hukumu hiyo kusomwa, Wakili wa utetezi,  Aloyce Komba amedai kuwa mshitakiwa hakuwahi kuvunja sheria  ya kijinai kwani alikuwa mwaminifu na hakuwahi kutoa siri ya nchi licha ya ukimbizi wake.
Komba pia ameongeza kuwa, tangu mteja wake apate kashfa hiyo, ameathirika kiuchumi kwa kuwa alitakiwa kustaafu miaka sita ijayo  lakini sasa anakosa mapato yake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...