Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Celestine Mwesigwa wamepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam na kusomewa mashtaka yanayo wakabili likiwemo la Kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa EXCOM imeridhia kubadilishwa kwa saini ya Bank,
Kufanya fojari ya risiti za kuwa Malinzi anaidai TFF (risiti zipo zaidi 20 zinazodaiwa kufojiwa) hii inamhusu Malinzi pekee
Na Mwisho ni shtaka la kutakatisha fedha dola za kimarekani zaidi ya laki tatu (hii inawahusu wote watatu ambao ni Malinzi, Mwesigwa na Nsiana). Watuhumiwa hao wamerudishwa rumande na kesi yao imepangwa kusikilizwa tena Julai 3, 2017. Taarifa kamili itawajia baadae kidogo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Pole sana Ndg Malinzi na wenzako! Do ni shida kweli kweli!!!
ReplyDelete