THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NHC TANGA YAWATANGAZIA KIAMA WANAOGUSHI FOMU ZA UPANGISHAJI

SHIRIKA la Nyumba la Taifa Mkoani Tanga (NHC) limewa tahadharisha watu wanaoghushi fomu za maombi ya kupangisha katika nyumba zao na kuziuza kwa wananchi kuacha mara moja tabia hiyo kwani watakabanika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa Shirika hilo,Mussa Kamendu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mipango mbalimbali ya shirika hilo ikiwemo kuzifanyia ukarabati nyumba wanazozimiliki ili ziweze kuwa katika muonekana mzuri kwa zile ambazo zimeonekana kuchakaa.

Alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi kughusi fomu ambazo zinatolewa na shirika hilo kwa kuzisambaza kwa wengine na kuwauzia jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliopo.

“Ukiangalia sisi kama shirika tumekuwa tukitoa fomu kwa wananchi ambao wanataka kupangisha kwenye nyumba zetu lakini katika hilo kumejitokeza baadhi ya watu wanazitoa kopi na kuziuza kitendo ambacho ni uvunjifu wa taratibu tulizoziweka “Alisema.

“Jambo hili ni hatari hasa kwa ustawi wa shirika letu kwani
linachangia kukosesha mapato hivyo tutahakikisha tunawa shughulikia watakaobainika kufanya hivyo bila kuangalia nafasi yake kwa maslahi ya ustawi wa shirika letu “Alisema Meneja huyo. 
Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha moja kati ya chemba ambazo zinafanyiwa ukarabati eneo la mtaa wa market Jijini Tanga na Fundi Mchundo wa Shirika hilo jana wakati alipotembelea kuona hali ya ukarabati huo unavyoendelea.
Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha waandishi wa habari maeneo mbalimbali waliokarabati
Mafundi wakiendelea na kazi kama wanavyoonekana
Meneja wa Shirika wa Shirika la Taifa la Nyumba Mkoani Tanga (NHC),Mussa Kamendu akikagua mitaro iliyochimbwa kwa ajili ya kupitisha mfumo wa maji taka.