Mashabiki wakiwa ndani ya Dar Live.


SIKU zikiwa zinahesabika kuelekea Usiku wa Nishushe Dar Live utakaofanyika Sikukuu ya Idd Mosi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar, wakali kibao watakaoliamsha dude siku hiyo wamefungukia makamuzi watakayotoa. 

Katika usiku huo, pazia la burudani litafunguliwa rasmi mapema kuanzia saa 8:00 asubuhi ambapo burudani ya watoto itatolewa chini ya kundi la sarakasi na kudensi la Wakali Dancers pamoja na Kundi la Muziki wa Asili la Makhirikhiri kutoka Tanzania. Wakizungumza na Mikito Nusunusu kwa nyakati tofauti, wakali hao watakaoongozwa na R.O.M.A Mkatoliki walisema kuwa wataliamsha dude mwanzo mwisho sambamba na kutoa sapraizi kibao jukwaani. ROMA “Kwa muda mrefu sijafanya shoo tangu nipate matatizo hapa kati. Mara ya mwisho nilifanya shoo Dar Live nikiwa na Darassa ilikuwa Usiku wa Michano (Mkesha wa Mwaka Mpya) na waliofika waliona na ambao hawakufika walisimuliwa. Safari hii nisingependa ikupite hii. Nimepona na nipo fiti hivyo mje kwa wingi kushuhudia shoo yangu ya kwanza tangu mwaka huu uanze nikikinukisha kwa ngoma kali kuanzia Viva Roma Viva, K, Ivan, Kaa Tayari na nyingine kibao.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...