Muonekano wa picha kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival. Benki ya NMB ilikuwa ni mmoja wa makampuni wadhamini.
BENKI
ya NMB Tanzania jana iliungana na Watanzania nchini kusherehekea Siku
Kuu ya Eid El Fitr kwa kuwa mmoja wa makampuni wadhamini wa tamasha
lililoandaliwa na kampuni ya Azam la Kids Circus Carnival ambalo
limehusisha watu wa aina mbalimbali kuanzia watoto na hata watu wazima
kufurahi kwa pamoja.
Tamasha
hilo ambalo linafanyika kwa siku mbili mfululizo yaani Eid Mosi (Juni,
26) na Eid Pili (Juni, 27) linafanyika katika viwanja vya Kenyatta
(Kenyatta Ground) vilivyopo Osterbay, jijini Dar es Salaam.
Katika
tamasha hilo lililokuwa na michezo anuai lilijumuisha huduma mbalimbali
ambazo zinazotolewa na Benki ya NMB ambapo watu waliohudhuria tamasha
walipata nafasi ya kujua huduma zinazotolewa na NMB, na pia kupata
nafasi ya kufungua akaunti.
Pamoja
na hilo pia kulikuwa na michezo mbalimbali ya watoto na maonesho ya
wanyama mbalimbali wakiwepo simba, chui, mamba, farasi, sungura na
wengine wengi. Zifuatazo ni picha mbalimbali za tamasha hilo. Watoto mbalimbali wakifurahia huduma kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival.
Watu mbalimbali wakifurahia huduma kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival Watoto mbalimbali wakifurahia huduma kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival. Baadhi ya michezo kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...