Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Banki ya NMB, Omary Mtiga akizungumza na zaidi ya watoto 450 waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam. NMB kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika wamefanikiwa kufuturisha watoto hao yatima kutoka vituo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Banki ya NMB, Omary Mtiga (wa pili kulia) akitoa zawadi kwa watoto walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine ikiwemo Benki ya NMB katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Shabaan Robert uliopo Upanga na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali pamoja na wadau waliosaidia kufanikisha jambo hilo wakiwemo NMB na wengine. Baadhi ya watoto waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika futari iliyoandaliwa na NMB kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...