THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAHIMIZA USHIRIKIANO NA WADAU

 Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Mdemu akitoa maelezo wakati wa Mkutano wa Kazi kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wadau  ( hawapo pichani)kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali zilizopo  Mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma. Madhumuni ya  Kikao kazi hicho ilikuwa ni  kukutana wa wadau hao kwa lengo la kujadiliana, kubadilishana mawazo na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali ambazo wadau hao pamoja na  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wanakumbana  nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.  Wadau walioshiriki kikao  hicho ni kutoka Mahakama,  Takukuru, Magereza, Polisi, Wakala wa Barabara, Maliasili, Halmashauri, Mawakili wa Serikali, Wanasheria na  wanajamii. Kushoto kwa   Naibu Mwanasheria Mkuu   Wakili Mfawidhierikali  Kanda ya Tabora Bw. Jackson Bulashi na kulia ni  Kamanda wa Takukuru Tabora  Bw. Fidelis Kalungura
 Sehemu ya  wadau ambao wamekuwa na  mazungumzo na majadiliano na Ujumbe wa  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa  Serikali  ulioongozwa na Naibu  Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bw. Gerson  Mdemu. Majadiliano hayo  yamefanyika katika ukumbi wa  mikutano wa Takukuru Mkoani Tabora siku ya  Ijumaa ( June 16) ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya  Wiki ya Utumishi wa Umma.
Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, Mahakama, Polisi, Takukuru, Maliasili, Magereza,  Halmashauri,  Wakala wa Barabara,Mawakili wa Serikali na Wanasheria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha majadiliano baina ya  wadau hao  na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa  Serikali ambapo  wameazimia kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho na kisha kupeana mrejesho. Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA