THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ORIFLAME YASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UTOAJI HUDUMA NA UUZAJI BIDHAA ZAKE ZA VIPODOZI DUNIANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kusheherekea miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili kushoto ni Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt, Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu.
Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt (wapili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra,Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu. 
Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina. 
Balozi wa bidhaa za Oriflame Tanzania, Missie Popular akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kutambulishwa na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo katika nchi za Afrika Mashariki, Mary Riungu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani.
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za Oriflame, wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi wakuu wa Kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY