NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka viongozi na watendaji wa zamani wa ngazi za matawi waliowania tena nafasi za uongozi katika uchaguzi unaoendelea hivi sasa ndani ya chama hicho kutoshiriki kwenye vikao vya kuchuja na kujadili fomu za wagombea wa nafasi za uongozi.

Tahadhari hiyo imetolewa na Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima katika mwendelezo wa ziara yake huko Mkoa wa Kusini kichama Unguja, alisema mtu aliyewania nafasi ya uongozi ndani ya chama hicho hana haki ya kujadili na kuchuja fomu za wagombea wenzake kwani kufanya hivyo ni kinyume na Katiba ya Chama hicho.

Alisisitiza kwamba katika zoezi hilo ni lazima kila kiongozi asimamie taratibu za uchaguzi ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa ya lazima.

“ Kuna baadhi ya matawi kumetokea changamoto za baadhi ya wagombea kujadili na kupitisha fomu za wagombea wenzao jambo ambalo ni kinyume na taratibu za Kikatiba hivyo hatuwezi kuvumilia vitendo hivyo ni bora uchaguzi urejewe katika maeneo yaliyoripotiwa ukiukaji wa miongozo yetu”, alisema Nd. Pereira.

Nd. Silima alisema dhamira ya chama hicho ni kuhakikisha chaguzi zote zitakazofanyika ndani ya chama na jumuiya kuhakikisha wanapatikana viongozi bora waliopatikana kwa mujibu wa matakwa ya Kikatiba na sio watu binafsi.Katibu huyo aliweka wazi msimamo wake kwamba atapambana vikali na baadhi ya watu waliopandikizwa katika uchaguzi huo ili wapange safu na makundi ya viongozi wanaowataka wao kwa baadhi ya ngazi za uongozi .

Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, kichama, Ramadhan Abdallah Ali “ Kichupa” mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Mkoa huo zilizopo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima akitoa nasaha kwa viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya za Kusini na Kati Kichama katika ziara ya kiongozi huyo visiwani Zanzibar.
Baadhi ya viongozi na Watendaji wa ngazi mbali mbali za Chama na jumuiya zake Mkoa wa kusini na Wilaya zake kichama. ( PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...