Mafunzo hayo ya siku mbili Juni 5 na 6, 2017, yanafanyika katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga, na yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3, TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, na wakufunzi kutoka mikoa mbalimbali ambako mradi unatekelezwa. 

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, alisema mfumo wa FFARS utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha kuwa vituo vya kutolea huduma vinakusanya na kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma bora. 

“Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Rais katika kutekeleza mpango wa elimu bila malipo aliamuru kuwa fedha za ruzuku za gharama za uendeshaji wa shule lakini pia vituo vya kutolea huduma zitapelekwa moja kwa moja katika vituo hivyo, hivyo basi usimamizi wa ruzuku hizo utafanywa na vituo husika,” alieleza Msovela. 

“Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo ili kuhakikisha kuwa vituo vyetu vya kutolea huduma kupitia fedha za ruzuku vinakuwa na mfumo maalum wa kuandaa taarifa za mapato na matumizi, hali ambayo itachangia uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi,” aliongeza Msovela. 

Aidha, alisema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na PS3 katika kuunganisha wadau, na kuongeza kuwa ni wakati mzuri watanzania wakaiga mfano wa nchi kama Marekani ambao wapo mbele zaidi katika masuala ya uwazi na utawala bora katika kuwapa taarifa wananchi zinazohusu maeneo yao. 
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, amefungua mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’.
Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akifungua mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga 
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akifungua mafunzo mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa kwa wakufunzi zaidi ya 130 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na kati waliohudhuria mafunzo hayo.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akizungumza ukumbini. Kulia ni Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago, na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...