THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SAKA SAKA 2017 YAFIKIA UKINGONI MJINI BAGAMOYO

​Kituo cha redio cha EFM Jumapili ya leo tarehe 25/6/2017 kimehitimisha mchezo wake uitwao sakasaka ambao ulianza mnamo tarehe 28 Mei na kuchezeshwa katika wilaya tano ambazo ni Kigamboni, Ubungo, Ilala, Temeke, na Bagamoyo. Ni mwaka wa tatu sasa tangu mchezo huu wa sakasaka uanze kuchezeshwa.
Mchezo huu huchezeshwa kwa kuficha vitu katika uwanja fulani na vitu hivyo huwa na thamani ya pesa iliyoandikwa katika karatasi yenye muhuri wa kituo cha redio, ambapo dondoo za kitu kilichofichwa na mahali kilipofichwa hutajwa katika redio hivyo msikilizaji atakae weza kuunganisha dondoo hizo na kukipata kitu hicho ndio atakuwa mshindi.
Efm redio imetoa kiasi cha shilingi milioni saba na laki tano katika mchezo huu wa sakasaka kwa washindi 40 katika wilaya zote tano ambapo katika kila wilaya wanapatikana washindi nane, thamani ya mshindi wa kwanza ni shilingi milioni moja, na washindi wengine ni wa laki moja, elfu hamsini n.k.
Imekua ni kawaida kama redio kuja na vitu mbalimbali ambavyo vitashirikisha wasikilizaji wetu ikiwa ni namna moja ya kuwashukuru na kuwawezesha katika biashara zao pamoja na familia zao kiujumla.
 Baadhi ya mashabiki wa EFM wakishuhudia zoezi zima na washindi kukabidhiwa pesa zao.
 Mtangazaji wa kipindi cha Uhondo ya E-fm radio, Adam Melele ( Swebe Santana) akimkabidhi mshindi wa kwanza Vaileth Rumishael Shayo kitita cha shilingi milioni moja.
 Adam Melele (Swebe Santana) akizungumza jambo na moja ya washindi wa saka saka Bw. Aibu Msomba
 Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Efm radio akimkabidhi Bw. Munir Hamidu moja wa washindi wa saka saka shilingi elfu hamsini.
Bi. Khadia Selemani akikabidhiwa kiasi cha shilingi laki moja baada ya kuibuka mshindi kwa kile alichokisaka kuwa sahihi na kinatoka E-Fm radio.