Kituo cha Efm redio kimekabidhiwa kiasi cha shilligi Milioni moja na laki tano (1,500,000/=) pesa taslimu kwa washindi mbali mbali walioshiriki katika mchezo wa saka saka (treasure hunt) leo tarehe 04/06/2017 kwa wakazi wa wilaya ya Ilala – Ukonga (Majumaba sita) katika kiwanja cha Gonga. Huu ni msimu wa tatu wa Saka saka tokea mchezo huu umeanzishwa na mwaka huu itafanyika katika wilaya tano, Kigamboni, Ilala, Ubungo, Temeke kwa Dar es salaam na Bagamoyo kwa wilaya ya Pwani.
 Denis Rupia( kulia ) mtagazaji wa E-fm radio akiwaanamuhoji moja ya mshiriki wa Saka saka (katikati)  na Aneth Mrindoko- Afisa matukio, uhusiano na mwasiliano (kushoto) akiwa anakagua kitu kilichotolewa na mshiriki kama ndicho kilichofichwa na Efm.
 Baadhi wa wananchi wa Ukonga wakishuhudia zoezi zima lililokuwa linaendelea.
 Baadhi ya washiriki wa Saka saka wakiwa wako tayari kwa ajili ya uhakiki wa kile walichokiokota ni kitu kilichokuwa kimefichwa na Efm redio.
 Lulu Riziki Magala ambae ni mshindi wa kwanza aliye ibuka na shilingi 1,000,000 pesa tasilimu za kitanzania.
 Moja ya washindi Mohamed Madiga akikabidhiwa kiasi cha shilingi elfu hamsini na Jesca Mwanyika - Afisa matukio, uhusiano na mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...