WASHIRIKI wa maonyesho ya 41 ya kimataifa ya biashara maarufu Sabasaba wametakiwa kutumia fursa ya maonyesho hayo kujifunza kutoka kwa washiriki wa kimataifa ili kuboresha bidhaa wanazozalisha. 
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Mhandisi Christopher Chiza wakati akifungua semina ya siku moja kwa washiriki wa maonyesho hayo iliyofanyika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.

 “Lengo la semina hii ni kuelekezana mawili matatu kwa lengo la kuboresha, lakini naomba nitumie fursa hii kuwaasa washiriki wa ndani kujifunza kutoka kwa wageni, wazalishaji asali kwa mfano lazima muangalie kwanini asali ya mwenzangu imegombaniwa sana kuna kitu gani nimekosea.

“Hii italeta tija na maana ya maonyesho itakuwa imezingatiwa, takwimu zinaonyesha asilimia kubwa ya wajasiriamali ni wamiliki waviwanda vidogo na vidogo kabisa ambavyo ni asilimia 99 ya viwanda vyote,” alisema Mhandisi Chiza. 
Alibainisha kuwa ipo haja ya kufanyika maboresho ya viwanja hivyo kwa sababu watu watachoka ku9ona mambo hayohayo kila msimu unavyofika, hivyo akasema serikali itajipanga ili kutanua maonyesho hayo kwa ngazi ya kanda. 
“Tunahitaji kubadilika kwa kuanzia eneo la viwanja, tuimarisha barabara na kujenga majengo ya kisasa ikiwemo hoteli za nyota tano ili washiriki wa kimataifa walale hapahapa na mamlaka ijiongezee kipato,” alisema Mhandisi Chiza. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bwana Rutageruka, alizungumzia umuhimu wa kujiimarisha kwa sababu ushindani umekuwa mkubwa kinyume na miaka iliyopita ambapo Sabasaba yalikua maonyesho pekee nchi nzima. Sabasaba ilikua kama Sikukuu ya Eid au X-Mass, kila mmoja alikua anasubiri kwa hamu msimu ufike, lakini kwa sasa maonyesho ni mengi na ushindani umekuwa mkubwa. Hivyo ipo haja ya kujitathmini na kuboresha baadhi ya maeneo na huduma,” alisema Bw. Rutageruka. 
Aliongeza kuwa kulingana na kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu yatakayoanza Juni 28 ni ‘Ukuzaji wa biashara kwa maendeleo ya sekta ya viwanda,’ washiriki watumie fursa hiyo kujitafutia soko la bidhaa wanazozalisha katika viwanda hivyo kwani hilo si eneo la kuuza bidhaa bali kujitangaza. 
Miongoni mwa watoa mada katika semina hiyo walikuwa ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ambapo Afisa udhibiti ubora wa shirika hilo Bibi Joyline Mwinuka alisema kila mwaka wanatoa mafunzo kwa washiriki wa maonyesho ya biashara kwa lengo la kuwaeleza umuhimu wa kuidhinishwa viwango vya bidhaa zao kwa lengo la kujiongezea soko na kulinda afya za wateja wao.

“Kazi kubwa tunayoifanya hapa ni kuwaelekeza wateja wetu umuhimu wa TBS na kujua kazi zake, pili maonyesho kama haya ya kimataifa yanavutia bidhaa nyingi za viwandani kutoka ndani na nje ya nchio lazima tujue ubora wao ukoje, hivyo ni wajibu wetu kutoa maelekezo na kufuatilia kilabidhaa inayoingia katika viwanja hivi,” alisema Bi. Joyline. 
Maonyesho ya Sabasaba kwa miaka mingi sasa yamekuwa chachu ya wazalishaji kutangaza bidhaa zao ambapo watu wengi hujitokeza kununua na kuangalia bidhaa na huduma zinazotolewa na washiriki.
Washiriki   kwenye  Maonyesho ya 41 ya Biashara  ya Kimataifa yatakayoanza rasmi tarehe 28 mwezi huu, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali kwenye semina elekezi ya  siku moja jijini Dar es Salaam ambayo iliendeshwa na waandaji wa maonyesho hayo Mamlaka  ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE),maonyesho  yatafanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
 Washiriki   kwenye  Maonyesho ya 41 ya Biashara  ya Kimataifa yatakayoanza rasmi tarehe 28 mwezi huu, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali kwenye semina elekezi ya  siku moja jijini Dar es Salaam 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka  ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka akisisitiza jambo  jijini Dar es Salaam jana wakati wa semina elekezi kwa washiriki wa Maonyesho ya 41 ya Biashara  ya Kimataifa  yatakayoanza rasmi tarehe 28 mwezi huu, kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius  Kambarage Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya  Mamlaka  ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Mhandisi Christopher Chiza  akizungumza  jijini Dar es Salaam jana wakati wa semina elekezi kwa washiriki wa Maonyesho ya 41 ya Biashara  ya Kimataifa  yatakayoanza rasmi tarehe 28 mwezi huu, kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius  Kambarage Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka  hiyo), Bw. Edwin Rutageruka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...