THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI

Benny Mwaipaja, WFM

Serikali imesema inaendelea kupitia sheria, kanuni na taratibu za misamaha ya kodi mwaka hadi mwaka ili kuhakikisha kuwa misamaha yote isiyokuwa na tija inafutwa na hivyo kuiwezesha Serikali kuongeza mapato kwa ajili ya kupeleka huduma za maendeleo kwa wananchi wake.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Masasi, Mhe. Rashid Mohamed Chuachua (CCM), aliyetaka kujua namna Serikali inavyodhibiti misamaha ya kodi tangu irekodiwe kwa viwango vya juu Mwaka wa Fedha 2011/2012.

Mhe. Chuwachuwa alihoji mwenendo wa utoaji wa misamaha ya kodi kwa wawekezaji kwa maelezo kuwa Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizopoteza fedha nyingi kwa ajili ya misamaha ya kodi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kigezo cha kuvutia Wawekezaji.

Alisema kuwa kwa mujibu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2009-2010, Tanzania ilipoteza asilimia 15 ya Pato la Taifa lililotarajiwa kukusanywa kutokana na misamaha ya kodi, mwaka 2010-2011 asilimia 8, kwa mwaka 2011-2012 asilimia 27 ya mapato ya Serikali yalipotea.

“Je hali ya misamaha ya kodi kuanzia 2013-2014 hadi sasa ikoje’’. Alihoji Mhe. Chuachua.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),misamaha ya kodi kama sehemu ya asilimia ya Pato la Taifa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013/14 hadi sasa imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka.