Serikali yaipongeza Tulia Trust kwa kusomesha vijana mafunzo ya Sanaa Bagamoyo Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imepongeza juhudi za Taasisi ya Kijamii ya Tulia Trust kwa kuwezesha kusomesha vijana 20 masomo ya Sanaa na Utamaduni katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) huku akiziomba taasisi za wadau wengine kuiga mfano huo. 
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya masomo kwa vijana hao 20 waliodhaminiwa na Tulia Trust, Kaim Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi. Leah Kilimbi,ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Wizara hiyo,amewataka vijana hao kuwa Mabalozi wazuri ili wakawafundishe na wengine kile walichojifunza hapo. 
“Sisi kama Serikali, tunafarijika sana kwa namna wadau wanavyosaidiana nasi katika kuleta maendeleo katika Nyanja mbalimbali. Taasisi ya Tulia Trust imeonyesha nia na tunaipongeza sana kwani imesaidia vijana wetu kujifunza Sanaa, Utamaduni na kila aina ya mafunzo. Tunaamini huko waendako watakuwa mabalozi wazuri sana pia wadau wengine waige mfano huu” alieleza Bi. Leah Kilimbi. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Gabriel Kiiza akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vyeti kwa vijana hao 20 waliofadhiliwa kwa msaada wa Tulia Trust. Tukio limefanyika chuoni hicho Juni 16.2017, Mjini Bagamoyo.
Balozi wa Tulia Trust Hassan Ngoma akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vyeti kwa vijana hao 20 waliofadhiliwa kwa msaad wa Tulia Trust. Tukio limefanyika chuoni hicho Juni 16.2017, Mjini Bagamoyo.
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Vijana hao wakikabidhi risala yao kwa uongozi wa Tulia Trust.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...