THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Sheikh Shariff amaliza Ziara yake jijini Arusha,kuelekea Tanga

 Sheikh Shariff Majini kutoka Dar es salaam leo Jumapili amemaliza ziara yake Jiji Arusha kwa kufanya mkutano mkubwa katika stendi ya Hiace jirani na Soko la Kilombero.

Ikumbukwe Sheikh alianza ziara Arusha siku ya Jumapili tarehe 28 May ambapo aliendesha Dua katika ukumbi wa C.C.M Mkoa.

Aliendeleabnq mkutano wa nje siku ya Jumamosi tarehe 03 Juni na amemaliza mikutano yake Jumapili tarehe 04 Juni kati viwanja vya stendi yaa Hiace jirani na soko lq Kilombero Jijini Arusha.

Jumatatu tarehe 05-06-2017 Sheikh ataanza ziara Mkoa wa Tanga ambapo Junamosi tarehe 10 Juni na Jumapili Juni atafanya mkutano mkubwa pamoja na mambo mengine atafanya Dua kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa saba mchana ili kuwahi kuandaa futru kwa akina mama.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Arusha waliojitokeza kwenye mkutano wa Sheikh Shariff Majini.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Arusha waliojitokeza kwenye mkutano wa Sheikh Shariff Majini.
Sheikh akiongoza dua pamoja na kuombea watoto waliofika mkutanoni.