Sheikh Shariff Majini siku ya Jumamosi tarehe 24-06-2017 sawa na Ramadhani 29 ataendesha Dua nzito kwa ajili ya kuuaga mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika ukumbi wa Star Light Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Dua hiyo ni maalum hasa kwa kina mama na itaafanyika kuanzia asubuhi saa mbili mpaka saa sita mchana ili kutoa fursa kwa wataohudhuria kuwahi kuandaa futari.
Mara baada ya kumalizika kwa Dua, Sheikh ataenda Jijini Arusha kwa mwaliko maalum wa Baraza la Eid siku ya Eid Pili. Baraza la Eid litafanyika katika viwanja vilivyopo jirani na soko la Kilombero na Stand ya Hiace Jijini Arusha.
Sheikh atarejea Dar es salaam mara tu baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...