THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Shindano la Sprite Bball Kings 2017  limeingia katika hatua ya 16 baada ya timu 52 kukipiga wikiendi hii ikiwa ni ufunguzi wa michuano hiyo.

Michezo hiyo 26 iliyochezwa katika viunga vya viwanja vya Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) na kuzikutanisha timu hizo 52 katika mechi 26 za mtoano na 16 kufanikiwa kuingia hatua inayofuata.

Akitoa tathmini ya michuano hiyo Mratibu wa Sprite Bball Kings Basilisa Biseko amesema kuwa hatua ya mtoano imefanyika wikiendi hii na timu 16 kufanikiwa kuingua hatua inayofuata ila katika mechi hizo kuna baadhi walipewa ushindi wa mezani.

Basilisa amesema kuwa kuna baadhi ya timu hazikufanikiwa kufika siku hiyo na  ratiba ilikuwa tayari imeshapangwa katika droo iliyokuwa imepangwa na kupelekea timu iliyokuwa imefika uwanjani kupatiwa ushindi wa mezani.


"Katika michezo 26 iliyochezwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya JMK Park timu 16 zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora, ila kuna timu zingine zimeingia kwenye hatua hiyo bila kucheza na timu pinzani kutokana na mpinzani wake kutokufika na kupelekea kupewa alama zitakazomruhusu kuingia hatua inayofuata,"amesema Basilisa.

Amesema kuwa, kwa timu zilizopata alama nyingi ndizo zilizofanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora na mashindano hayo yataendelea tena ili kumpata mshindi wa Sprite Bball Kitaa kwa mwaka 2017.

 Timu zilizofuzu kuingia hatua ya 16 bora katika shindano la Sprite Baball Kings 2017 ni DMI, Dream Chaser, UDSM, Oysterbay, Ukonga Warriors, The Fighter, Ardhi na Bongo Hits.Timu zingine ni Chanika Legends, Montfort, Heroes S/B, Kigamboni Heroes, TMT, Mchenga, Kurasini na Landforce.

Mashindano ya Bball Kings mwaka huu yanadhaminiwa na Sprite wakishirikiana na kituo cha East Africa Redio na TV  na yalizinduliwa mapema mwezi wa tano na kuanza usaili kwa wilaya za Teemek, Kindondoni na Ilala na kupata timu 4.52 zilizojitokeza kushiriki shindano hilo.
Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mtanange wao.
 Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM (jezi ya njano) wakipambana katika hatua ya mtoano ya shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
 Mashabiki na timu zingine zilizoshiriki katika  hatua ya mtoano ya shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) wakiwa jukwaani wakifuatilia baadhi ya michezo mingine.
Timu za mpira wa kikapu wakiwa wanachuana katika shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano wa chama Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) na Mratibu  wa Sprite BBall Kings Manase Zablon  (kushoto) akiwa pamoja na mtangazaji wa East African Drive David Rweganyira wakichambua baadhi mechi zilizokuwa zikiendelea.